Wahenga wa kale walinena kuwa atangaye na jua hujuwa. Baada ya mwezi mmoja baada ya Social Good Summit 2014,nimekuwa nikiwaza na kuwazua jinsi teknologia na mtandao inaweza kusaidia kubadilisha tabia na kupata suluhisho kwa matatizo ya kimataifa.
Lakini hata kabdla kutarajie kubadili mienendo na tabia zinazokera kabisa,ni lazima tukubali na kuwa na ufahamu wazi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu, ukosefu wa usawa wa kijinsia na pia ukosefu wa usalama kwa watoto na akina mama.Ni lazima tuwe wangalifu kuhusu pia unyanyasaji dhidi ya wanawake, ukosefu wa elimu haswa kwa wasichana na pia ukosefu wa huduma za afya.Ni lazima raia wawe na suluhisho dhidhi ya shida zinazo kumba ukosefu wa uwezeshaji wa kiuchumi na pia ukosefu wa uraia.
Matatizo na maswala haya ni lazima tuyatatue na tuyapambane nazo kwa sababu zinazuia maendeleo.Kwa mfano ,kila siku wasichana na akina mama dunia nzima wanakumbana na hali hatari katika jamii zao.Wasichana wachanga wanaolewa na kina babu,na wanawake wanadhulumiwa hapa na pale.Inashangaza kuwa wanawake haswa wanaotoka kwa jamii na ulimwengu zinazoendelea hawataruhusiwa kupata elimu.Je ni kompyuta watakayo pewa sasa?
Jamii nyingi hata waleo hupatia mtoto wa kiume faidha na mapendeleo chungu nzima.Familia ikibahatika kama mtende, sana sana huchangia kwa maendeleo ya wavulana na wanaume wenzio peke yao.Lakini nikijiuliza ni jinisi ipi tutakayo badilisha uongo huu na kupigania haki ya wasichana na akina mama ninakeuka na kuamini kwamba safari hii si ya msichana wala akina mama peke yao!Badala kubadilisha tabia na mawazo ni jukumu ya jamii nzima inayokumba wazee kwa vijana na watoto kwa wazazi na watu wote wa jinsia zote.
Tukirejea Social Good Summit na jukumu yetu kupigania haki za binadamu wote,nimegundua kweli kwamba umoja ni nguvu.Jamii inayofuria kuona msichana mchanga akipata elimu haiwezi kubadilika kwa siku moja au baada ya mkutano wa kimataifa kama ya UNGA,CSW au hata Social Good Summit.Pole pole ndio mwendo na ni lazima tupate washujaa kwa umbali na urefu kusaidia jamii kama hii kusonga mbele.Ni muhumu pia kupata wavulana na wazee wanao kubaliana na ajenda na mawazo ya usawa ya wanawake na wanaume.Ni muhimu sana kupata wasemaji wanaoweza kubadilisha matamaduni kutoka ndani.
Nikikumbuka Social Good Summit 2014,ninajawa na buraha na furaha kwa sababu watu wengi kutoka pembe tofauti tofauti ya dunia wamekubaliana na mawazo yangu kwamba ni lazima sote tushiriki kutatua matatizo yetu na ni muhimu haswa kuwakilisha na kunenea wale ambao bado sauiti zao haziskizwi!